Showing posts with label News. Show all posts
Showing posts with label News. Show all posts

Friday, February 24, 2012

Mtumishi Freddy Chavala Kuanza Season One Ya Matamasha ya Cheka Tena(Laugh Again Concert ) Tar 4 March 2012,Pale Landmark Hotel,Ubungo,Dsm.


 Baada ya mafanikio makubwa ya uzinduzi wa matamasha hayo mwishoni mwa mwaka jana, Nov 20 2011 pale Crystall hall ndani ya Blue pearl hotel, Ubungo plaza. Sasa mbeba IDEA
PRESIDENT CHAVALA  ameamua kuanza rasmi MSIMU WA KWANZA(SEASON ONE) wa matamasha hayo ya stand up comedy Tanzania, na Tamasha la kwanza ndio hili LAUGH AGAIN CONCERT One One litakalofanyika pale Ibungira hall ndani ya LANDMARK HOTEL,Ubungo,river side, jumapili ya kwanza ya march(4th March 2012), kuanzia saa nane na nusu mchana mpaka mbili usiku(2:30pm‐8pm).

 Mbali na CLOWN CHAVALA,Tamasha hili la Ubungo litawapandisha comedians chipukizi watano ambao ni Senior ABBY, GERALD MREMA, RICHARD CHIDUNDO, JOSEPHINE LUKWETO na MC MANU a.k.a Pilipili ya Sherehe toka Dodoma,Makundi mengine ya watu watakaonogesha tamasha hili ni pamoja na kundi maarufu la vijana waimbaji waitwao GLORIOUS CELEBRATION BAND, pia DAR ES SALAAM GOSPEL BAND, VOCAPELLA GROUP, VICTOR ARON,MADAM RUTH &CHRISS na wengine wengi bila kusahau kundi la DANCE.

Glorious Celebration Nao Watakuwepo Kumsindikiza Chavala

Akiongea na VIPAJI HALISI kutoka jijini Dar es salaam mbeba maono hayo Presdent Chavala amesema LAUGH AGAIN CONCERT One One litahusisha Stand Up Comedy(Zaidi), pamoja na Acapella, Dance,Sebene,Story telling, Zawadi & Suprises, Open Mic,Drama,na mengine mengi yatokanayo! Mbali na hayo kutakuwa na uzinduzi wa FORUM iitwayo QUALITY‐LOVE.com, ambayo itakuwa maalumu kwa ajili ya kujadili maswala ya Upendo safi kwa kina,ubora,upana na ubora wake katika nyanja mbalimbali za maisha ya binadamu. Na kama mambo yataenda kama yalivyopangwa kutazinduliwa kitabu kiitwacho "NO MORE SCHOOL FOR YOU"(Your birth was your Graduation) By FREDY E. CHAVALA.

Kiingilio kwa tamasha hili itakuwa 5000/= kwa tiketi, ambazo zinapatikana Victory Christian Centre(VCC);Tarakea Restaurant(Mwenge),Silver Spoon and Tausi Fashion pale Mlimani City,Global Publisher na Praise Power Radio pia mtu anaweza kununua tiketi kwa M‐Pesa (0753 883 797) au Tigo Pesa (0713 883797) kwa kutuma 6000/= na atapata tiketi yake mlangoni, lakini hakikisha unatuma pesa kwa namba yako mwenyewe iliyosajiliwa kwa jina lako!


The Voive,Waimbaji wa Acapella Nao watakuwepo

















 LAUGH AGAIN CONCERT Season One itakuwa na matamasha nane katika mikoa mitano ya hapa nchini kwa kuanzia, Matamasha haya yatafanyika kuanzia March‐August/September 2012 katika mikoa ya Dar es salaam(3),Arusha(1),Mwanza(1),Dodoma(2) na Mbeya(1).

 Tar 1st April ni ARUSHA na 29th April ni ndani ya COLD CREST HOTEL,Mwanza then DSM tena !
Clown Chavala,The King of Stand up Comedy! Alimaarufu kama President Chavala!
Ambaye ni MC Maarufu ,Mchekeshaji(stand up comedian) na Muasisi wa christian stand up comedy Tanzania, ambaye ndiye Mchekeshaji mkuu na Project manager wa hii project,amesema matamasha haya yatakuwa endelevu na yatafika katika kila mkoa wa Tanzania na baadae mwaka huu tunategemea kuanzisha vipindi maalum katika televisheni kadhaa nchini na mbeleni zaidi kutunza matamasha hayo katika DVDs. Zaidi mwaka huu tutakuwa na Movie project ambazo zitawahusisha vipaji vipya kabisa sana sana katika tasnia ya Stand Up Comedy.

Wednesday, December 7, 2011

Saadi Gaddafi 'ajaribu kupenya Mexico'


Saadi Gaddafi
Serikali ya Mexico imesema imezuia njama iliyokuwa ifanywe na kundi la wahalifu la kumpenyeza kwa magendo mmoja wa watoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi nchini Mexico.
Saadi Gaddafi amekuwa kwenye kifungo cha nyumbani nchini Niger iliyopo Afrika Magharibi tangu alipoikimbia Libya mwezi Septemba.
Msemaji wa serikali ya Mexico alisema Saadi Gaddafi na baadhi ya wanafamilia wake walizuiwa kutokana na matokeo ya ripoti za kijasusi.
Watu wengi wamekamatwa kutokana na tukio hilo.
Maafisa wa Mexico wamsema jaribio hilo- lililoibuliwa Septemba 6- lilihusisha majina na nyaraka za uongo.

Waziri wa mambo ya ndani Alejandro Poire alisema mpango huo unahusisha mtandao wa uhalifu " mkubwa wa kimataifa", lakini ikagundulika mwezi Septemba kabla ya mpango huo kukamilika.


Mtandao huo ulihusisha watu kutoka nchi mbalimbali, ikiwemo Mexico, Denmark na Canada, Bw Poire aliuambia mkutano wa waandishi wa habari huko Mexico.
Alisema, walikuwa wakinunua nyumba zenye salama na kufungua akaunti za benki.
Tarehe 14 Septemba- siku nane baada ya njama hiyo kugundulika- Niger ilisema Saadi Gaddafi, mwenye umri wa miaka 38, aliwasili mjini Niamey.
Iliripotiwa kuwa alisafirishwa kwa ndege ya kijeshi kutoka mji wa Agadez kaskazini mwa nchi hiyo.

Septemba 29, Shirika la polisi la kimataifa, Interpol lilitoa " hati ya kukamatwa" kwa Saadi Gaddafi, wakitaka nchi wanachama imkatae iwapo atatokea kwenye nchi zao.
Wakala wa polisi wa kimataifa wamesema anatakiwa kwa madai ya kutoa vitisho kwa kutumia silaha alipokuwa mkuu wa shirikisho la mpira la Libya.

Saadi Gaddafi, ambaye alikuwa akicheza soka katika ligi kuu ya Italia Serie A, pia amewekewa vikwazo vya kusafiri na mali zake kutiwa tanji chini ya azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa lililopitishwa mapema mwaka huu.